Ninaweza kupata ujauzito nikijamiiana nikiwa kwenye hedhi yangu?
Jibu fupi: NDIO!
Wazo la kwamba huwezi kupata ujauzito wakati upo kwenye hedhi yako ni dhana potofu iliozoeleka. Hata hivyo, ingawa kitakwimu inaweza ikawa ngumu kutokea, bado inawezekana kabisa!
Hii inawezekanaje?
Kuna njia kadhaa za kupata ujauzito ukiwa kwenye hedhi yako, aidha iwe kwa bahati tu, mizunguko mirefu au mifupi zaidi ya upevukaji mayai, au hedhi isiyo na utaratibu!
Uwezekano wa kupata ujauzito huamriwa na mzunguko wako wa upevukaji mayai. Uwezekano mkubwa zaidi wa mwanamke kushika ujauzito hujikita kwenye wakati gani hupevusha mayai, au hutoa yai. Kiuhalisia, hili hutokea katikati ya hedhi na hedhi, hivyo kama mzunguko wako ni wa siku 28, na siku ya 1 ndio siku ya mwanzo wa hedhi yako, unaweza kutarajia kiujumla kupevusha yai kwenye siku ya 14. Hata hivyo, hata pamoja na uwezekano kuwa mkubwa zaidi kwenye siku ya 14, uwezekano wa kupata ujauzito nje ya kipindi hiki ni wa 100%.
Kuwa na mzunguko mfupi au mrefu zaidi kuliko wa wastani kunaweza pia kuongeza uwezekano wa kupata ujauzito wakati wa hedhi yako. Kwa mfano, kama tukiangalia mzunguko wa upevushaji yai mfupi zaidi kuliko wa wastani inawezekana kupevusha yai siku 4-5 tu baada ya kumaliza hedhi yako. Mbegu ya kiume inaweza kuishi ndani ya mfuko wa uzazi wa mwanamke kwa hadi siku 5, hivyo inawezekana kabisa kuwa mbegu ya kiume bado itakuwa hai kama ulijamiiana kwenye hedhi yako na halafu ukapevusha yai ndani na siku zilizofuata au kwenye wiki ya hedhi yako.
Mwisho, hedhi isiyo na utaratibu inaweza kufanya ikawa ngumu kufuatilia tarehe yako ya kupevusha yai. Aidha imekuwa haina utaratibu muda wote au imekuwa haina utaratibu kutokana na mkazo au vichocheo na/au mabadiliko ya uzito, hedhi isiyo na utaratibu inaweza kufanya upevushaji yai usiwe wa kutabirika.
Basi, ni wakati gani salama zaidi kujamiiana bila kupata ujauzito?
Ijapokuwa unaweza kufuatilia mzunguko wako wa upevushaji yai na kujaribu kujamiiana nje ya muda ambapo yai hutolewa, bado ujauzito unaweza kutokea muda wote. Kwa mfano, ikiwa umejamiiana mwishoni mwa hedhi yako, lakini ikatokea umepevusha yai mapema, kuna uwezekano kwamba ukashika ujauzito. Njia salama zaidi ya kuepuka ujauzito ni kwa kutumia njia za uzazi wa mpango kama kupangilia uzazi au kwa kutumia kondomu na vitendo vingine vya ngono salama!
Unataka kujifunza zaidi? Una maswali mengine kuhusu kujamiiana, maambukizi ya magonjwa ya zinaa yaani STIs, UKIMWI, au uzazi wa mpango? Kumbuka unaweza kuchati na Nivi kwenye WhatsApp na Facebook Messenger muda wowote. Ni mazungumzo binafsi, ya usiri, na bure!
Comments