askNivi inafanya kazi kwa hatua 3 rahisi:
HATUA YA 1:
Bonyeza kiunga cha Nivi kuanza kuzungumza. WhatsApp au Messenger yako itafunguliwa moja kwa moja na utaona neno kwenye sanduku la maandishi.
HATUA YA 2:
Tuma neno hili ili nijue tunapaswa kuzungumza kuhusu nini.
HATUA YA 3:
Nitakuuliza maswali machache, tafadhali jibu ili niweze kukujua vizuri kidogo na nikupendekeze chaguo bora kwako. Kisha endeleza maongezi!
Ukweli, sio Hadithi
Nivi ni kama shangazi yako mzuri ambaye ana majibu yote na hakuhukumu. Nivi anakupa ukweli ili uweze kuamua ni nini kinachokufaa
Mapendekezo ya Kibinafsi
Mwambie Nivi umri wako, jinsia na mahali unapoishi ili kupata mapendekezo ya kibinafsi. Nivi inaweza kukusaidia kupata mbinu ya kupanga uzazi inaofaa kwa mwili wako.
Pata Kliniki
Ni muhimu sana kuwa na kliniki nzuri. Nivi inaweza kukusaidia kupata eneo iliyo karibu nawe ili uweze kupata mbinu ya kupanga uzazi iliyo salama na ya kibinafsi wakati unahitaji.
Nivi ni Bure, Salama na ya Kibinafsi
Ni rahisi kuzungumza. Nivi inapatikana 24/7.